TANGAZO LA ZABUNI NA. AAM/EQT/DOM/02/2024

TANGAZO LA ZABUNI NA. AAM/EQT/DOM/02/2024 YA UUZAJI WA DHAMANA ZA WADAIWA WA EQUITY BANK (TANZANIA) LIMITED

Kwa maelekezo tuliyopewa na mteja wetu Equity Bank (Tanzania) Limited Makao Makuu Ohio Street, Golden Jubilee Tower, Third Floor, S.L.P 110183 Dar Es Salaam, Tunauarifu umma kwamba tutauza kwa zabuni, nyumba za wadaiwa wa benki hiyo kama ilivyoanishwa hapa chini:-

Loti: Loti No. 1
Aina ya Dhamana/Mali: Landed Property
Maelezo ya Dhamana / Mahali Ilipo: Nyumba Makazi iliyopo kiwanja Na. 77, CT Na.24204 - DLR, LO Na. 96253 / 18844, Kitalu 'B' Eneo la Chichadi East, Manispaa ya Dodoma.

VIGEZO NA MASHARTI YA ZABUNI
1. Waombaji wanaotaka kununua mali tajwa wanashauriwa kupata taarifa Zaidi za mali hiyo kutoka ofisi ya Adili Auction Mart Limited iliyopo Nyumba Na. 53, Kiwanja Na. 151, Kitalu 45C Kijitonyama, Eneo la Makumbusho, Dar Es Salaam.

2. Ukaguzi na wa dhamana husika utafanywa na wazabuni wenye nia ya kununua kabla ya kuwasilisha zabuni zao kuanzia tarehe ya tangazo hili mpaka siku ya kufungua zabuni.

3. Nyaraka za zabuni zinapaswa kuwa katika bahasha isiyo na rangi na jalada la nje limeandikwa Zabuni Na. AAM/EQT/DOM/02/2024 ya ununuzi wa dhamana za wadaiwa wa Equity Bank (Tanzania) Limited, ikileleza nambari ya loti na kuwasilishwa kwenye ofisi ya Adili auction Mart Limited.

4. Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha zabuni itakua alhamisi tarehe 12/09/2024 saa 4 kamili asubuhi na kufunguliwa siku hiyo hiyo mbele ya wazabuni au wawakilishi wote saa nne asubuhi kwenye ofisi ya Adili Auction Mart Limited.

5. Zabuni Zitakazotumwa kwa njia ya telegraph, faksi, barua pepe au kuwasilishwa nje ya muda hazitapokelewa.

6. Equity Bank (Tanzania) Limited ina haki ya kupokea au kukataa zabuni yoyote na haina wajibu wa kueleza sababu za kupokea au kukataa zabuni yoyote.

7. Mshindi wa Zabuni lazima alipe angalau 25% ya bei ya zabuni ndani ya saa 48 baada ya kujulishwa kuwa mshindi wa zabuni, Asilimia 75 iliyobaki lazima ilipwe ndani ya siku kumi na nne (14) tangu siku ya malipo ya awamu ya kwanza.

8. Iwapo mshindi atashindwa kulipa salio la 75% iliyobaki ya kiasi cha zabuni ndani ya muda uliowekwa, kiasi kilichowekwa kitatwaliwa na mali itauzwa tena kwa zabuni mpya baada ya tangazo jipya kutolewa.

9. Mali inauza kwa misingi ya “Kama ilivyo na mahali ilipo”.


KWA MAELEZO ZAIDI, TAFADHALI PIGA SIMU YOYOTE KATI YA ZIFUATAZO
0767 873 988 / 0744 149 080 / 0782 031 111 / 0716 651 103
E-MAIL: info@adiliauction.co.tz